Field Marshal Muthoni wa Kirima

Tata Nduta anasimulia hadithi ya msichana aliyeota juu ya uhuru wa kweli

Ardhi kuibwa, ndimi zenye sumu na safari ya kishujaa!

Katika kipindi hiki cha KaBrazen, Tata Nduta anasimulia hadithi murua inayohusu msichana aliyeota juu ya uhuru wa kweli. Katika ulimwengu wa kutisha ambapo vyura wasio na rangi wala nyoyo wamenyakua ardhi na hata kubadili nyoyo za watu wake, Muthoni mdogo kamwe hakati tamaa. Muthoni anatukumbusha kwamba hatua kwa hatua, hata sisi tunaweza kufikia uhuru wa kweli kwa kutokata tamaa katika kutimiza ndoto zako.

Zingatia kwa makini: Kupigwa shoti ya umeme kunatajwa na pia dhuluma ya kimwili dhidi ya mtoto.

Bora kwa watoto wenye umri wa miaka 4 hadi 9 na wote wanaopenda hadithi.

Kipindi hiki ni cha dakika 22 na sekunde 53.

Tueleze mafikira yako ukitumia #KaBrazen

SIFA:

Mwandishi- Anne Moraa

Matafiti - Laura Ekumbo, Aleya Kassam, Anne Moraa

Muigizaji wa sauti- Afrikan Njogu (Tata Nduta)

Mchoraji - Chela Yego

Mzalishaji msaidizi - Mweru Gitau

Mzalishaji wa Sauti- Wambui Waciuri for Za Kikwetu Productions

Wimbo wa mada- Timothy Arinaitwe & Mbogua Mbugua & Laura Ekumbo

Nembo - Francis Ally Mlacha

Mkurugenzi wa Sauti- Laura Ekumbo

Mwandishi Mkuu- Aleya Kassam

Mkurugenzi wa Ubunifu- Anne Moraa

KaBrazen Consortium - Sifa Kamili: Nthanze Musyoka • Jane Mumbanu • John Muya • Laura Ekumbo • Aleya Kassam • Anne Moraa • Wilma Mosoti • Chela Yego • Afrikan Njogu • Monity Odero • Wambui Waciuri • Packson Ngugi • Melissa Mbugua • Josephine Kiarani • Allan Wasega • Mweru Gitau • Marcus Olang • Narmin Kassam • Molly (YRD) • Beliya Ndhlovu Bukuru (YRD) • Benjamin Mboya • Janet Haluwa • Zosi Kadzitu • Miriam Kadzitu • Jake/John Njoka • Kevin Kaesa

Asante kwa Ciru Ngigi, Too Early For Birds: Brazen Edition Team, Ngartia, Owaahh, Abu, Gathoni & The Aga Khan University.

Shukraani maalum kwa the late Field Marshal Muthoni wa Kirima.


Kusanyiko hili la pili la hadithi za sauti za KaBrazen inapigwa jeki na ruzuku ya Ignite Culture chini ya mradi ACP-EU Culture (Afrika Mashariki) Hazina hii inatekelezwa na HEVA kwa ushirikiano na baraza la Uingereza nchini pamoja na mchango wa kifedha kutoka kwa muungano wa Uingereza ,na vile vile msaada zaidi kutoka kwa muungano wa ACP , hizi ni (Nchi za Afrika, Karibea, na Pasifiki) Ni sehemu ya mradi wa kimataifa wa ACP-EU Culture.

Previous
Previous

Angelique Kidjo

Next
Next

Mariama Sonko