Bonus (LIVE) Zarina
Tata Nduta anasimulia hadithi moja kwa moja Siku ya Mashujaa
Katika kipindi hiki cha ziada cha KaBrazen, tunamsikia Tata Nduta akisimulia hadithi moja kwa moja! Katika hafla ya KaBrazen Live Experience iliyofanyika siku ya Mashujaa, Tata Nduta alisimulia hadithi ya kusisimua ya jinsi Zarina Patel, msichana aliyekuwa na moyo mkubwa, alivyopigana kwa ujasiri kuokoa bustani ya Jeevanjee jijini Nairobi, dhidi ya kugeuzwa kuwa maegesho ya magari. Katika siku hii maalum, Tata Nduta alipata furasa ya kusimulia hadithi hii moja kwa moja mbele ya kikundi cha watoto kama tu wewe, na mgeni maalum kabisa…Zarina Patel Mwenyewe!
Bora kwa watoto wenye umri wa miaka 4 hadi tisa na wote wanaopenda hadithi.
Kipindi hiki ni cha dakika 28 na sekunde 13.
Tueleze mafikira yako ukitumia #KaBrazen
SIFA
Mwandishi- Aleya Kassam
Mtafiti - Laura Ekumbo, Aleya Kassam, Anne Moraa
Muigizaji wa Sauti - Afrikan Njogu
Mchoraji - Chela Yego
Mzalishaji msaidizi - Mweru Gitau
Mzalishaji wa Sauti- Wambui Waciuri for Za Kikwetu Productions
Wimbo wa mada- Timothy Arinaitwe & Mbogua Mbugua & Laura Ekumbo
Nembo - Francis Ally Mlacha
Mkurugenzi wa Sauti- Laura Ekumbo
Mwandishi Mkuu- Aleya Kassam
Mkurugenzi wa Ubunifu- Anne Moraa
KaBrazen Consortium - Sifa Kamili: Nthanze Musyoka • Jane Mumbanu • John Muya • Laura Ekumbo • Aleya Kassam • Anne Moraa • Wilma Mosoti • Chela Yego • Afrikan Njogu • Monity Odero • Wambui Waciuri • Packson Ngugi • Melissa Mbugua • Josephine Kiarani • Allan Wasega • Mweru Gitau • Marcus Olang • Narmin Kassam • Molly (YRD) • Beliya Ndhlovu Bukuru (YRD) • Benjamin Mboya • Janet Haluwa • Zosi Kadzitu • Miriam Kadzitu • Jake/John Njoka • Kevin Kaesa
Asante kwa Zarina Patel & Zahid Rajan, Too Early For Bids: Timu ya Brazen, Watoto waliohudhuria hafla ya KaBrazen Live, Marilyn Kamuru na Aga Khan University.
Kusanyiko hili la pili la hadithi za sauti za KaBrazen inapigwa jeki na ruzuku ya Ignite Culture chini ya mradi ACP-EU Culture (Afrika Mashariki) Hazina hii inatekelezwa na HEVA kwa ushirikiano na baraza la Uingereza nchini pamoja na mchango wa kifedha kutoka kwa muungano wa Uingereza ,na vile vile msaada zaidi kutoka kwa muungano wa ACP , hizi ni (Nchi za Afrika, Karibea, na Pasifiki) Ni sehemu ya mradi wa kimataifa wa ACP-EU Culture.