Ketty Nivyabandi

Msichana aliyeota kwa sauti.

Ndoto zinazomezwa, rangi zinazotoweka na mpango bora kabisa!

Katika kipindi hiki cha KaBrazen, Tata Nduta anasimulia hadithi ya kusisimua juu ya msichana anayeota kwa sauti. Katika ulimwengu ambapo ndoto za watu zinamezwa na kinyonga mlafi, Ketty kwa ujasiri, anawaonyesha watu wake wa Burundi umuhimu wa kuendelea kuota! Ketty anatukumbusha, ndoto zenu ni muhimu sana, kwa hivyo usimruhusu mtu yeyote akuzuie kuota!

Ni bora kwa watoto wenye umri wa miaka 4 hadi 9 na wote wanaopenda hadithi.

Kipindi hiki ni cha dakika 21 na sekunde 18.

Tueleze mafikira yako ukitumia #KaBrazen

SIFA:

Mwandishi- Aleya Kassam

Mtafiti - Nthanze Musyoka

Muigizaji wa sauti - Afrikan Njogu (Kiswahili - Tata Nduta)

Mchoraji - Chela Yego

Mzalishaji msaidizi - Mweru Gitau

Mzalishaji wa sauti- Wambui Waciuri wa Za Kikwetu Productions

Wimbo wa mada - Timothy Arinaitwe & Mbogua Mbugua & Laura Ekumbo

Nembo - Francis Ally Mlacha

Mkurugenzi wa sauti - Laura Ekumbo

Mwandishi mkuu - Aleya Kassam

Mkurugenzi wa ubunifu - Anne Moraa

KaBrazen Consortium - Sifa kamili: Nthanze Musyoka • Jane Mumbanu • John Muya • Laura Ekumbo • Aleya Kassam • Anne Moraa • Wilma Mosoti • Chela Yego • Afrikan Njogu • Monity Odero • Wambui Waciuri • Packson Ngugi • Melissa Mbugua • Josephine Kiarani • Allan Wasega • Mweru Gitau • Marcus Olang • Narmin Kassam • Molly (YRD) • Beliya Ndhlovu Bukuru (YRD) • Benjamin Mboya • Janet Haluwa • Zosi Kadzitu • Miriam Kadzitu • Jake/John Njoka • Kevin Kaesa.

Asante kwa Ketty Nivyabandi, Marilyn Kamuru na Aga Khan University.

Kusanyiko hili la pili la hadithi za sauti za KaBrazen inapigwa jeki na ruzuku ya Ignite Culture chini ya mradi ACP-EU Culture (Afrika Mashariki) Hazina hii inatekelezwa na HEVA kwa ushirikiano na baraza la Uingereza nchini pamoja na mchango wa kifedha kutoka kwa muungano wa Uingereza ,na vile vile msaada zaidi kutoka kwa muungano wa ACP , hizi ni (Nchi za Afrika, Karibea, na Pasifiki) Ni sehemu ya mradi wa kimataifa wa ACP-EU Culture.

Previous
Previous

Nelly Cheboi

Next
Next

Bi Kidude